Jaji wa New York amepanga tarehe 15 Aprili ya kesi ya Donald Trump katika kesi ambayo itakuwa ya kwanza ya jinai inayomhusisha rais wa zamani, inayohusisha madai kwamba alighushi rekodi za biashara wakati wa kampeni ya urais 2016.
Jaji Juan M. Merchan alitoa uamuzi huo Jumatatu, lakini sio kabla ya kuwakashifu mawakili wa rais huyo wa zamani alipokuwa akipima wakati wa kupanga upya kesi hiyo, baada ya kutupwa kwa hati kwa dakika za mwisho na kusababisha kuahirishwa kwa tarehe ya awali.
Merchan alikuwa amekasirishwa na kile alichopendekeza kuwa madai ya utetezi yasiyo na msingi ya “makosa ya mwendesha mashtaka.”
Timu ya utetezi ya Trump, ambayo iliitisha rekodi hizo mwezi Januari, haikuleta wasiwasi kuhusu hati zinazoweza kukosekana wiki mapema.
“Kwa nini ulisubiri hadi miezi miwili kabla ya kesi kusikizwa? Kwa nini hukuifanya mwezi Juni au Julai [2023]?” Merchan alimuuliza Todd Blanche, wakili wa Trump.
Trump amekana mashtaka ya kughushi rekodi za biashara hadi sasa .
Waendesha mashtaka wa Manhattan wanasema Trump alifanya hivyo kama sehemu ya juhudi za kulinda kampeni yake ya 2016 kwa kuzika kile anachosema kuwa hadithi za uwongo za ngono nje ya ndoa na inadaiwa watu watatu walipokea malipo hayo: mlinda mlango wa zamani wa Trump Tower; mwigizaji wa ponografia Stephanie Clifford, a.k.a. Stormy Daniels; na Karen McDougal, aliyekuwa Playboy Playmate of the Year.