Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Manyara imesikiliza kesi namba 05 ya mwaka 2021 ya uhujumu uchumi inayowakabili watu wanne baada ya kukutwa na meno 13 ya Tembo ambayo ni Nyara ya serikali katika kijiji cha Moyamayoka wilayani Babati ambayo ni sawa na kuawa kwa Tembo Saba.
Hata hivyo mahakama hii ya hakimu mkazi mkoa wa Manyara imekwisha muhukumu kutumikia kifungo cha miaka 20 jela Bernad Masalu ambaye alikuwa ni kati ya washtakiwa waliokutwa na meno hayo ambayo ni nyara ya Serikali.
Kwa sasa mahakama kwa mara nyingine imesikiliza kesi hiyo kwa upande wa wshitakiwa wa tatu ambao ni Yenderson Masumbuko, Ramadhani Swalehe pamoja na Mwajuma Athuman ambapo kwa mujibu wa ushahidi wa upande wa jamhuri mashahidi wameielezea mahakama kuwa meno hayo yalikutwa kwenye nyumba aliyokuwa akilala Ramadhani Swalehe huku bi Mwajuma akijumuishwa kwenye kesi hiyo kutokana na yeye kuwepo mazingira ya tukio ikiwa yeye ndugu na mshitakiwa Yenderson.
Mara baada ya ushahidi kutolewa na upande wa Jamhuri Mahakama kupitia hakimu mfawidhi mwandamizi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Manyara Simon Kobelo akatoa nafasi ya washitakiwa kuuliza maswali na baadaye kesi hiyo kuahirishwa hadi tarehe 14 mwezi huu kwaajili ya kusikiliza utetezi wa upande wa washitakiwa.
Wakati huo huo mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Manyara imeondoa kesi namba 19 2021iliyokuwa inawakabili raia watano wa Malawi ambao walikamatwa mnamo 15.04.2021kwa kuingia nchini bila kuwa na vibali kinyume cha sheria namba 45 ya makosa ya uhamiaji ya kuingia nchini pasipokuwa na kibali.