Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) Jaji wa rufani, Barke Sehel amesema kesi za ubakaji na wanaume kuingiliwa kinyume na maumbile zimekuwa nyingi kiasi cha wao wenyewe kujiuliza ni kwanini.
“Kesi za ubakaji tunapoenda kila mkoa zipo, enzi za zamani ulikuwa unasema kwenye mikoa fulani ukienda hata sisi kwa upande wa rufaa tunaenda kusikiliza katika ile mikoa, tulikuwa tunasema ukienda mkoa fulani kule hutokosa mashauri ya ubakaji na ukienda mkoa fulani lazima kule kesi zake za mauaji ila sasa hivi hii trend ipo kila mkoa inasikitisha sana, kesi za ubakaji ni nyingi sana hatujui ni maadili ama ni nini,”.
“Nyingine ni kuingiliwa kinyume na maumbile watoto wa kiume zipo kesi nyingi katika mikoa ambayo hutegemei kwa kweli inasikitisha,” amesema Jaji Sahel wakati akizungumzia Maadhimisho ya miaka 25 ya TAJWA ambayo yatafanyika jijini Arusha Januari 19-23,2025 huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan.