Juzi zilitangazwa bei za tozo za kila gari litalopita juu ya daraja jipya la Nyerere Kigamboni ambapo kuanzia Baiskeli, Pikipiki na Magari kila kitu kitakua na bei yake, baadhi ya wakazi wa Kigamboni wakataka ufafanuzi zaidi kama mtu anapita mara mbili kwa siku akienda kazini na gari yake.
Mfano magari madogo yanayotumika sana na watu binafsi yatatakiwa kulipia shilingi 1500 kila yanapopita juu ya daraja hili lakini kwenye taarifa ya kwanza haikufafanua kama mtu analipia kwa siku ama kwa kila anapopita na ndio maana baadhi ya Wakazi wa Kigamboni walitaka kujua kama kwa wao kuna punguzo lolote hasa wanaopita zaidi ya mara moja kwa siku.
Injinia Karim Mattaka ambaye ni Meneja kwenye mradi wa daraja hili ameongea na AyoTV na kusema bei zilizotajwa ni za kupita mara moja hakuna utaratibu mwingine zaidi ya hapo, utalipia kwa kadri unavyopita hata kama ni mara sita kwa siku utalipia safari zote sita.
Kwa alichokisema Injinia hapo juu ni wazi kabisa hakutokua na punguzo maalum au huruma kwa baadhi ya Wakazi wa Kigamboni ambao walipaza sauti zao kupitia mitandao ya kijamii kuhusu kufikiriwa kwakuwa watapita mara nyingi kwa siku juu ya daraja hilo, zaidi unaweza kumtazama Injinia kwenye hii video hapa chini.
ULIKOSA KUTAZAMA HATUA ZA MWISHO ZA UJENZI WA DARALA LA KIGAMBONI? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE