Siku mbili zilizopita Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangalla aliliagiza Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua wafanyabiashara wanne vigogo ndani ya siku saba kwa tuhuma za mauaji ya mwanaharakati wa uhifadhi wa tembo Wayne Lotter August 16, 2018 vinginevyo atalipeleka suala hilo kwa Rais John Magufuli.
Leo January 26, 2018 Jeshi la Polisi kupitia Msemaji wake Barnabas Mwakalukwa limesema wamesikia agizo hilo la Waziri Kigwangalla lakini Jeshi la Polisi halifanyi kazi kwa shinikizo bali kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za Jeshi hilo.
“Hatufanyi kazi kwa matamko ya bungeni, alichokisema Kigwangalla nimekisoma kwenye vyombo vya habari akihusisha na suala la mwanaharakati aliyeuawa, sisi hatufanyi kazi kwa kufuata vyombo vya habari vimeandika nini au limetolewa tamko gani au kuna shinikizo gani, tunafanya kwa kufuata taratibu zilizopo.” – Kamanda Barnabas Mwakalukwa
BREAKING: JPM ATOA MILION 15 YA MATIBABU YA WASTARA
Baada ya kuachiwa kwa dhamana nje ya Mahakama Tido na Kubenea