Leo April 3, 2018 Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikuku ni kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Fidelice Mbaruku Simbagungile Mafumiko kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali.
Uteuzi wa Dkt. Mafumiko umeanza April 3, 2018.
Kabla ya kuteuliwa Dkt. Mafumiko alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW)
Dkt. Mafumiko anachukua nafasi ya Prof. Samuel Manyele ambaye amemaliza muda wake.
“Nawaona Mawaziri wengine wanabeba ndoo za maji”- Rais Magufuli