Leo May 30, 2019 Nakusogezea story inayomhusu Tikiko Furugutu anayeishi Mkoani Kigoma amejitokeza na kuomba msaada wa matibabu ya ziada baada ya kuumwa ugonjwa usiojulikana kwa takribani miaka 13 bila ya kupona.
Tikiko anaeleza kuwa alipata ugonjwa huo alipokuwa akioga katika Bwawa la Maji na ambapo aling’atwa na kitu asichokijua na ndipo vidonda vilipoanza kujitokeza katika miguu na mikono yake ambapo jitihada mbalimbali za kimatibabu zimefanyika bila ya mafanikio.
Anasema alipoenda Hospitali ya Wilaya ya Kasulu baada ya vipimo hawakupata ugonjwa wowote hivyo walimpatia dozi ya ugonjwa wa Ukoma ambapo hadi leo haijaonyesha matumaini yoyote huku hali yake ikizidi kubadilika na kuwa mbaya hata zaidi.
RC HAPI “MA-MC, WAPIGA PICHA WANATAKIWA VITAMBULISHO MACHINGA ILA SIO WENYE LESENI”