Zaidia ya watu 235 kati ya watu 6858 wamegundulika kuwa na ugonjwa wa Homa ya Ini baada ya vipimo vilivyofanywa katika Vituo vya Afya katika kipindi cha mwezi December 2018 na July 2019 Mkoani Kigoma.
Hayo yameelezwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dr. Poul Chaote ambapo ameeleza kuwa jamii inapaswa kuwa makini na ugonjwa huo ambao ni wakuambikiza kutokana na kuwa hatari zaidi ya Ugonjwa wa UKIMWI.