Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe amekamilisha ziara ya siku nne Singida, Tabora, Shinyanga na Geita ambapo amefanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa Mnadani na kuwajumuisha wananchi wa Katoro na Buseresere mkoani Geita.
akizungumza katika mkutano huo Rais Magufuli amewaagiza viongozi wote kuanzia ngazi ya Mkoa hadi Kitongoji hapa nchini kufuatilia matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kutoa elimu bila malipo kwa lengo la kudhibiti mianya ya matumizi mabaya ya fedha hizo.
Katika agizo hilo Dkt. Magufuli amewaonya walimu ambao wameanza kufanya udanganyifu kwa kuandikisha idadi kubwa ya wanafunzi kuliko idadi halisi kwa lengo la kupata mgao mkubwa wa fedha za ruzuku na amesema Serikali itachukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayebainika kufanya hivyo.
>>>’Ninafahamu mgao wa fedha hizo hutolewa kulingana na idadi ya wanafunzi waliopo, wapo baadhi ya walimu ambao wameanza kuandika wanafunzi hewa katika shule zao, ili kusudi aletewe hela nyingi kuliko idadi ya wanafunzi waliopo, wanafunzi kama wapo laki nne yeye anasema shule yangu hii ina wanafunzi laki tano, ili kusudi hela zikija za wanafunzi laki tano, za wanafunzi laki moja wagawane’
>>>’Napenda nitoe wito kwa walimu Tanzania nzima, mnatafuta matatizo, narudia mnatafuta matatizo, msijaribu kula hela ya Serikali’
ULIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI VS JAMES LEMBELI SHINYANGA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI