Serikali ya Saudi Arabia siku za hivi karibuni imetangaza kutenga Dola za Marekani Bilioni 64 ambayo ni sawa na Tsh Trilioni 153.6 za Kitanzania kwa lengo la kukuza tasnia ya burudani nchini humo katika kipindi cha miaka 10 ijayo.
Kiongozi wa sekta ya burudani Ahmed bin Aqeel al-Khatib ameeleza kuwa serikali imepanga kufanya warsha 5,000 kwa mwaka 2018 na tayari ujenzi wa ukumbi wa kwanza wa burudani nchini humo umekwisha anza katika mji wa Riyadh.
Kwa mabadiliko haya serikali ya nchi hii inalenga kuboresha uchumi na kuzuia taifa hilo kutegemea mafuta ambapo kwa mwezi December 2017, iliondoa marufuku ya sinema za biashara.
Ahmed bin Aqeel al-Khatib aliviambia vyombo vya habari kuwa mpango huo unahitaji kuwa imeajiri watu 220,000 katika sekta ya burudani ifikapo mwishoni mwa mwaka 2018 kutoka watu 17,000 mwaka uliopita.
Ufafanuzi wa Kamanda Msangi, watu kupingwa nondo Mwanza.
Ili CCM Arusha ifanye mambo Kidigitali Mbunge Magige Akabidhi Kompyuta 28