Tatu Mzuka leo october 30 2018 wametangaza kutoa zaidi ya milioni 330 kwa mamilionea 28 ndani ya siku 4. Washindi hawa wametokana na jackpot kubwa za Tatu Mzuka zilizofanyika jumapili na jumatano wiki iliyopita na kuonyeshwa mubashara nchi nzima.
Usiku wa jumapili Bwana Jonas Qwaray Bura kutoka Babati, Arusha aliibuka kuwa milionea mpya nchini baada ya kushinda milioni 250 huku milioni 10 ikienda kwa washkaji zake 10, upande mwingine Bwana Jumanne Singani alijishindia milioni 50 siku ya jumatano huku milioni ikigawiwa kwa washkaji zake 10.
Baadhi ya washindi walikuwepo katika mkutano na waandishi wa habari kutoa simulizi za ushindi wao. Mshindi wa milioni 50 ambaye ni Bwana Jumanne Singani kutoka Dar-es-salaam aliishukuru Tatu Mzuka kwa kubadilisha maisha yake kupitia droo hizi kubwa tangu alipoanza kucheza.
“Tangu nianze kucheza Tatu Mzuka mwaka jana nimeshinda zaidi ya milioni 100 kupitia droo mbalimbali. Nimeweza kuwekeza katika biashara, kununua magari, pamoja na nyumba. Kwa ushindi huu nitaweza kupiga hatua zaidi kimaendeleo”-Singani.
Tatu Mzuka imekuwa ikitengeneza washindi kupitia droo za kila dakika 10, Mzuka ATM na washindi wa jackpot za jumapili na jumatano ambapo lazima mamilionea wanne wapatikate katika droo hizo.
Katika tukio la kuwatambulisha washindi, Mkurugenzi wa kitengo cha mawasiliano wa Tatu Mzuka Bwana Sebastian Maganga alisema furaha yao ni kuona watanzania wakifaidika na mchezo huu.
Ni furaha tu! Mshindi wa MILIONI 300 Tatu Mzuka alivyozipeleka kwao Mbagala, Bonyeza play hapa chini kuitazama