Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga amelieleza Bunge kwamba wapo baadhi ya Walimu wa vyuo vikuu nchini ambao wamekuwa na tabia ya kuwafelisha kwa kusudi wanafunzi na kisha kuwaomba rushwa ya ngono ili wawasaidie, Mlinga pia amemwambia Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichako kwamba yupo tayari kumpelekea majina ya Walimu hao.
“Kumekuwa na tatizo la wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu, Kuna walimu ambao wanajulikana kwamba wao ndio vidume vya mbegu kazi yao ni kuwafelisha wanafunzi na kutaka rushwa ya ngono. Waziri nitashirikiana na wewe nikuletee majina ya Walimu hao” –Goodluck Mlinga
Adhabu utayopata ukikamatwa umetupa uchafu Dodoma