Club ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC Jumapili ya November 4 2018 ilifanya mkutano wake mkuu sambamba na uchaguzi mkuu wa mwenyekiti na wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Simba SC ambapo kura zilihesabiwa hadi alfajiri ya November 5 2018.
Simba SC sasa inahesabika kama kampuni baada ya kufanikiwa kuingia katika mfumo wa mabadiliko ya uwekezaji wa hisa, ambapo mfanyabiashara Mohammed Dewji ndio alishinda Zabuni ya uwekezaji ndani ya club ya Simba hivyo maamuzi ya timu hiyo kwa sasa yatakuwa yanajadiliwa ndani ya bodi.
Baada ya uchaguzi kufanyika Swed Mkwabi ambaye alikuwa ndio mgombea pekee wa nafasi ya uenyekiti amepita bila kupingwa kwa zaidi ya asilimia 90 ya kura zote (kura 1579), hata hivyo washindi wa nafsi za ujumbe wamepatikana watano ambao ni Asha Baraka, Hussein Kitta, Dr Zawadi Kadunda, Mwina Kaduguda na Selemani Said.
Kaduguda alivyowakataa Waandishi baada ya matokeo ya Uchaguzi Simba SC