Baada ya sintofahamu ya muda mrefu hatimae leo February 4 2019 kikosi maalum cha uokoaji kimekuja na jibu kuhusiana na kupotea kwa ndege ndogo aliyokuwa amepanda mshambuliaji mpya wa Cardiff City Emiliano Sala akiwa na rubani wake David Ibbotson kupotea katika rada January 22 2019.
Msako wa kutafuta ndege hiyo uliendelea leo kwa kushirikiana vikosi vya uokoaji vya majini na vikosi vya uokoaji vya anga na kuendeleza msako maalum wa kuitafuta ndege hiyo iliyopotea zaidi ya siku 12 zilizopita, taarifa zilizoripotiwa usiku huu ni kuwa ndege hiyo imeonekana ikiwa imepata ajali na walikuwa wawili tu katika ndege hiyo Emiliano Sala na rubani wake David Ibbotson.
Taarifa zilizoripotiwa na mtandao wa Sky Sports ni kuwa vikosi vya uokoaji tayari vimetoa taarifa kwa familia za mchezaji na rubani huyo, Emiliano Sala alipotea katika ndege ndogo January 22 ambapo kabla ya kufikia leo ilikuwa inahisiwa kuwa ilipata ajali na wao kupoteza maisha, Sala alikuwa anatokea Nantes kurudi Cardiff City ambapo ndio alikuwa amejiunga nayo January hii kwa dau la pound milioni 15 lakini imeonekana ndege pekee ila Sala na rubani wake wanahisiwa kupoteza maisha.
Michael Wambura sasa kumpeleka Mahakamani Wallace Karia wa TFF