Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kwamba Serikali inaingia kwenye awamu ya pili ya uendeshaji wa mabasi ya mwendokasi Dar es salaam ambapo itatafuta mbia mwingine wa kushindana na aliyepo sasa ili kuweka changamoto kwa wabia wote na endapo ikibainika mwendeshaji wa sasa ana amatatizo Serikali itamuondoa.
Waziri mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni Abdallah Mtulia aliyehoji Serikali imejipanga vipi kuboresha mfumo huo wa usafirishaji.
Serikali yamjibu Halima Mdee kuhusu bomba la mafuta