Usiku wa January 25 2019 club ya Arsenal ilikuwa mwenyeji wa Man United katika wa Old Trafford kucheza mchezo wao wa FA Cup, Man United walikuwa wanaingia katika uwanja huo wakiwa na kocha wao wa mpito Ole Gunnar Solskjaer na hawajapoteza mchezo chini yake.
Wakati Arsenal wao wakiwa chini ya kocha wao Unai Emery, ikiwa inaaminika wako nyumbana na kuweza kufanya chochote dhidi ya Man United, timu ya Arsenal imejikuta ikipokea kipigo cha magoli 3-1 wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani magoli ya Man United yakifungwa na Alex Sanchez dakika ya 31, Jesse Lingard dakika ya 33 na Anthony Martial dakika ya 82.
Kufuatia ushindi huo walioupata Man United chini ya kocha wao wa mpito Ole Gunnar Solskjaer ambaye alirithi mikoba ya kocha Jose Mourinho, wanaendeleza rekodi yao ya unbeaten toka wamekuwa chini ya Ole Gunnar Solskjaer wakicheza game 8 na kushinda game zote nane.
VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”