Kamati ya maandalizi ya mbio za riadha za Heart Marathon 2018 safari hii imekutana na waandishi wa habari ikiwa ni wiki kadhaa zimepita toka wabadilishe tarehe ya mashindano hayo kutoka April 26 hadi 29 lengo likiwa ni kuboresha maandalizi ya michuano hiyo.
Mbio hizo ambazo zitafanyika April 29 zitaanzia Coco Beach na washindi mbali na zawadi ya fedha pia watazawadiwa medali ya ushindi wa mbio kwa watakaomaliza mbio hizo kwa watakaoshindana upande wa mbio za Baiskeli na riadha umbali wa Kilometa 21.1.
Pia kutakuwa na mbio za Kilometa 10, mbio za umbali wa Kilometa 5 lakini pia kutakuwa na umbali wa mita 700 kwa ajili ya mbio za watoto.
VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao