Pep Guardiola amefunguka kuhusu utamaduni wa Manchester City ambao umevunjwa mwaka huu kutokana na mwenendo mbaya wa klabu hiyo.
Kufuatia kushindwa na Aston Villa wikendi, City wameshinda mara moja pekee katika michezo yao 12 iliyopita katika michuano yote na wameshuka hadi nafasi ya saba kwenye Premier League.
Kwa hivyo, Guardiola ametoa wito kwa wachezaji wake kujitolea katika kipindi chote cha sikukuu ili kujaribu kubadilisha hali yao mbaya, ambayo inamaanisha kufanya mazoezi Siku ya Krismasi.
Hatimaye hii ni kwa ajili ya pambano la Boxing Day nyumbani kwa Everton kuliweka akilini.
Ingawa sio kitu ambacho wachezaji wa City wamezoea katika misimu ya hivi karibuni.