Hali ya taharuki imetanda katika kata ya Embaseni wilayani Arumeru Mkoani Arusha, baada ya mnyama aina ya kiboko kuvamia makazi ya watu nakujeruhi watu pamoja nakuharibu pikipiki zao.
Mwenyekiti wa kijiji cha maji ya chai Masa Mbise,amesema alimuumiza kijana aliyekuwa kwenye pikipiki kwa kuutenganisha mguu wake baada ya mnyama huyo kujificha kwenye mahindi.
“Ameweza kumg’ata mtu mmoja mguu nakuukata amevunja pikipiki mbili ikiwemo ya kwangu aliipigisha chini ,wakati anafukuzwa kwenye mahindi akamg’ata jamaa mmoja mgongoni akamchania nguo”- Masa Mwenyekiti
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro ametoa pole kwa wananchi waliojeruhiwa nakusema mnyama huyo ametoa kwenye hifadhi nakuwataka wananchi kuwa waangalifu na kwamba kwa sasa hakuna mnyama mwingine aliyebaki.