Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Mohamed Mussa maarufu kama Kibosile amekamatwa kwa madai ya kuwa tapeli sugu ambaye amekuwa akighushi nyaraka mbalimbali bandia za Serikali na ambazo sio za Serikali kwa kutumia mihuri mbalimbali na kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.
“Vitendo hivyo vimekuwa vikichafua taswira ya Serikali, amekamatwa na mihuri mbalimbali 24, vyeti vya kuhitimu sekondari, vyeti vya masomo ya sekondari, vyeti vya hati za tabia njema za Jeshi la Polisi, vibali vya uraia kwa wageni nchini, mihuri ya Taasisi za Serikali na binafsi kama Wizara ya Mambo ya Nje, UDSM, Manispaa ya Ilala, CRDB, NMB, STANBIC BANK, Rita, Wanasheria, Maafisa Watendaji, Polisi na Idara mbalimbali”
“Amekamatwa pia na kadi za Bank mbalimbali 16, Scanner 2 za kughushi nyaraka, hati mbalimbali za kusafiria (Passport) 33 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)”
“Mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa kwa kushirikiana na Taasisi nyingine na atafikishwa Mahakamami taratibu zitakapokamilika”———Muliro