Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipata huko.
Moja kati habari zilizoandikwa kwenye magazeti ya Tanzania ni hii ya kutoka gazeti la Jambo Leo yenye kichwa acha habari ‘Watanzania wengi ni vichaa, kila mmoja kati ya wanne ana tatizo hilo’
#JamboLEO UTAFITI: Kila watu wanne duniani, mmoja ana matatizo ya afya ya akili, 2015 TZ ilikuwa na wagonjwa 311,789 waliokwenda hospitali pic.twitter.com/M4UF68W4bW
— millardayo (@millardayo) October 11, 2016
Gazeti la Jambo leo limeripoti kuwa Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, watoto na wazee, Ummy Mwalimu amesema utafiti unaonesha kuwa kwa kila watu wanne duniani , mmoja ana matatizo ya afya ya akili.
Kwa mujibu wa Waziri Ummy wananchi wanapaswa kuwa makini kuchunguza afya zao za akili kwa sababu utafiti wa shirika la afya duniani ‘WHO’ zinaashiria kuwa jamii kwa sasa inakumbwa na maradhi mengi ya namna hiyo, Waziri Ummy alibainisha
>>>’Miongoni mwa watu wanaopata matatatizo ya kiakili ni wachache tu ambao wanaweza kufikia na kupata huduma ya afya ya akili, hata hao wanohudhuria vituo vya afya, ni wachache wamekuwa wakipata huduma stahiki’
Alifafanua sababu za kijamii zinazoweza kusababisha mtu kupata magonjwa ya akili ni umaskini uliokithiri, kutengwa na kubaguliwa na jamii. sababu nyingine alizitaja kuwa ni kunyanyaswa kimwili na kingono, kuwa tegemezi, kupoteza mali, kazi, ulevi, kukosa huduma muhimu na unyanyapaa.
Source: Jambo Leo
Unaweza kupitia habari zingine kubwa kutoka kwenye magazeti ya Tanzania leo
#HabariLEO Jitihada za JPM kubana matumizi yasiyo ya lazima serikalini, ambazo alihamishia EAC zimewezesha kuokoa zaidi ya bil 1.2 pic.twitter.com/JOscAPQ5R6
— millardayo (@millardayo) October 11, 2016
#NIPASHE NSSF yadai Serikali trilion 1 kwa miaka 10, yaanza kulipa kupitia hati fungani ambazo zitawezesha shirika kupata faida 10% hadi 18% pic.twitter.com/ISeLCQWbdN
— millardayo (@millardayo) October 11, 2016
#MWANANCHI Miaka 22 ya wafanyakazi 31 wa BoT kutafuta haki yao iligubikwa na umaskini, maradhi na vuta nikuvute ya migogoro ya kisheria pic.twitter.com/QK2cBeVqsB
— millardayo (@millardayo) October 11, 2016
#MWANANCHI Walimu 18 wahojiwa kipigo cha mwanafunzi mbeya, majalada ya watuhumiwa 8 kupelekwa kwa mwanasheria wa serikali kwa hatua zaidi pic.twitter.com/tVadNJCbaz
— millardayo (@millardayo) October 11, 2016
#MWANANCHI Mfumuko wa bei kwa September, mwaka huu umepungua mpaka kufikia asilimia 4.5 kutoka 4.9 ya August pic.twitter.com/cyBJc3j8nI
— millardayo (@millardayo) October 11, 2016
#MWANANCHI Lissu atumia saa 2 kutetea ubunge wa Bulaya kwa kumbana maswali Wassira ktk shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Bunda pic.twitter.com/Hz5dhFkkgL
— millardayo (@millardayo) October 11, 2016
#MWANANCHI Mahakama kuu imebariki maombi ya CUF ya kumfungulia kesi msajili wa vyama vya siasa pamoja na Prof. Lipumba pic.twitter.com/Jy1sJprKIL
— millardayo (@millardayo) October 11, 2016
#MTANZANIA Watu 472 waliohukumiwa adhabu ya kifo wanasubiri saini ya Rais Magufuli ili kujua hatima ya utekelezaji wa adhabu zao ama laa pic.twitter.com/Pt3RxDZvhb
— millardayo (@millardayo) October 11, 2016
#MTANZANIA Imeelezwa kwamba Tanzania ina wagonjwa wa akili 450,000 huku DSM ikiongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi ikifuatiwa na Mwanza pic.twitter.com/xguxuuK8pF
— millardayo (@millardayo) October 11, 2016
#JamboLEO Vifaa vya kuhakiki vyeti kwa watumishi na kuandikisha vitambulisho vya taifa vyaibiwa Kishapu Shy, baadhi ya watumishi wahojiwa pic.twitter.com/upme13XXVA
— millardayo (@millardayo) October 11, 2016
#UHURU Wizara ya fedha na Mipango imeanza uhakiki wa wastaafu wanaolipwa kupitia wizara hiyo mkoani Pwani pic.twitter.com/uImMrxPSvg
— millardayo (@millardayo) October 11, 2016
#UHURU Serikali kuanzisha akaunti maalumu za dawa ktk halmashauri zote ili kudhibiti matumizi ya fedha zinazotolewa kwaajili ya suala hilo pic.twitter.com/y2thZQhziz
— millardayo (@millardayo) October 11, 2016
#MAJIRA CCM Z'bar imesema haina mpango wa kufanya mazungumzo au makubaliano na CUF kuhusu uchaguzi uliopita pic.twitter.com/gr9GRywxrn
— millardayo (@millardayo) October 11, 2016
#NIPASHE Wakati kukiwa na taarifa za uhaba wa dawa ktk bohari kuu ya dawa 'MSD', Serikali imetoa taarifa ikisema zipo za kutosha pic.twitter.com/uLC9vwbXNA
— millardayo (@millardayo) October 11, 2016
ULIKOSA HII YA WAZIRI WA AFYA KUTAJA SABABU ZA KUNUNUA DAWA INDIA NA SI KENYA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI