Watoto huwa wanakuwa na fikra huru zaidi, mara nyingi kwa kuwa wanakuwa hawana uoga wala hawajui sheria, vyote hivyo hujifunza wakati wakiwa wanakua.
Ilikuwa ni mashindano ya kuandika katika shule yao, yeye akaona aandike hivi kwa Rais wa China; “… Uncle Xi, upunguze uzito kidogo wa mwili wako, unatakiwa uwe na mwili kama wa Obama. Hata kama ukiwa kama Putin sio mbaya …”
Ujumbe wake ukaendelea hivi; “… Marekani na Russia.. Ulaya na India wanapanga kwenda sayari ya Mars… na sisi tuharakishe…”
Ujumbe huu haukuwa rasmi, mwalimu wake amesema ilikuwa ni homework waliyopewa shule ambapo kila mwanafunzi anaambiwa aandike barua kwa mtu yoyote, kuhusu kitu chochote anachojisikia, lakini ikapata umaarufu baada ya baba yake kuiweka mtandaoni.
Kutokana na sheria kali za China barua hiyo iliondolewa mtandaoni muda mfupi baadaye kitu ambacho kimempa baba yake hofu kwamba huenda ikawa na athari kwa familia yake au mtoto wake kimasomo, japo anaamini mambo binafsi ya familia yake yataheshimiwa.
Nitafurahi ukiniandikia comment yako mtu wangu, unadhani watoto wa Bongo wakiambiwa wamuandikie Rais JK chochote watamuandikia nini?
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook