Toka kuanza kwa Utekelezaji wa Sheria Ndogo ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018, Benki Kuu ya Tanzania BOT imeendelea kuwafahamisha wasimamizi wa vikundi vinavyojishulisha na utachangishaji wa fedha vikiwemo VIKOBA kuwa ni makosa kutosajiliwa kwa vikundi hivyo na benki hiyo.
Akizungumza kwenye Semina ya Waandishi wa Habari Afisa Mkuu Mwandamizi kutoka Idara ya Usimamizi wa Idara ndogo za Fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Deogratias Mnyamani amesema ni kosa kisheria na atakayebainika kuendesha shughuli iyo kinyume na kufuata sheria atakumbana na sheria ya kwenda jela miaka miwili au kifungo kisichozidi miaka mitano.
“Kwa wanaofanya Biashara ndogo kwa Upande wa Vikundi bila ya kua na usajili wakibainika watakua na faini ya shilingi zisizopungua Millioni kumi na kifungo cha miaka isiopungua miwili na isiozidi mitano au vyote hivi kwa Pamoja yani faini na Kifungo —Deogratias Mnyamani “