Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, linamshikilia Michael Mbata (34), mfanyabiashara mkazi wa Dar es Salaam kwa tuhuma ya kujipatia Sh Milioni 150 kwa njia ya udanganyifu.
Akizungumza a wanahabari leo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi, alisema mtuhumiwa huyo alijipatia kiasi hicho cha fedha kutoka kwa Abdallah Huwel na lsaya Edward, wote wakazi wa Iringa.
Wakati Huwel alitapeliwa Sh Milioni 100 kwa ahadi ya kuagiziwa gari aina ya How, Bukumbi alisema Edward naye alitapeliwa Sh Milioni 50 kwa ahadi ya kununuliwa aina hiyo hiyo ya gari.
“Mtuhumiwa huyo aliwatapeli watu hao kwa ahadi ya kuwaagizia magari hayo kutoka Japan a Uingereza kupitia kampuni yake ya FOA Motors iliyopo Dar es Salaam, alisema.