Leo February 24, 2020 Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 23 amehukumiwa kifungo cha miezi nane gerezani na Mahakama ya Mji wa Kapenguria, Jimbo la Pokot Magharibi nchini Kenya kwa kosa la kumuingilia ng’ombe.
Mtuhumiwa huyo aliyejulikana kwa jina la John Pkemei aliripotiwa kutenda kosa hilo mnamo Oktoba 19, 2019 katika eneo la Kaibos lililopo katika Kaunti hiyo.
Imeelezwa kuwa siku ya tukio ilikuwa ni katika mashindano ya soka ambapo akiwa katika hali ya ulevi, alikuwa akitembea kabla ya mchezo kuanza alikutana na kundi la ng’ombe wakiwa malishoni ndipo alimvamia mmoja wa ng’ombe hao na kumuingilia.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo aliieleza mahakama kuwa alimuona mtuhumiwa akifanya tukio hilo na kwenda kuwataarifu watazamaji waliokuwa wakisubiri mechi, walipokwenda walimkuta mtu huyo akiendelea na kitendo chake ndipo walimkamata na kuanza kumpiga.
Polisi walikuja kumuokoa na kumpeleka kituoni na kusubiri ripoti ya daktari wa wanyama na baadaye alifunguliwa mashtaka.
Hakimu wa Mahakama ya Kapenguria, Godfrey Okwengu amesema kuwa uchunguzi uliofanyika umethibitisha mmtuhumiwa kuhusika na tukio hilo na alidhamiria kulitenda, hivyo hukumu aliyopewa ni sahihi.