Paul Siria ni kijana aliyeacha kufanya kazi ya uchimbaji wa madini ya Tanzanite kwenye mgodi wa Bilionea Saniniu Laizer nakuamua kumtumikia Mungu kwa njia ya nyimbo ambapo ali-trend baada ya kumtungia bilionea huyo nyimbo alipopata madini ya Tanzanite yenye thamani ya shilingi Billion 7.8 ambayo aliyauza serikali.
“Leo nimefanya uzinduzi wa albam na Bilionea ameweka mkono wake,nilikuja kuendelezaa karama yangu ambayo Mungu amenipa”-Siria
Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.KT) Dkt Fredrick Shoo amembariki kijana huyo baada yakuzindua albam yake nakusema kila mtu amewekwa kwa kusudi lake na kwamba kijana huyo kusudi la Mungu halikuwa kwenye machimbo bali Mungu alitaka kumtumia.