Usiku wa kuamkia tarehe 23 mwezi huu wa nne lilitokea tukio lisilo la kawaida katika eneo la Kagoma lililopo Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera ambapo inadaiwa Kijana Albert Masala mwenye Miaka 32 alitekwa na watu wasiojulikana kisha wakamtelekeza porini huku wakiwa wamemtundika msalabani ambapo aliokolewa na wasamalia wema asubuhi
Habari njema ni kwamba kijana huyo anaendelea vizuri na kupitia Ayo Tv na millardayo.com amesimulia tukio zima lilivyokuwa sambamba na mambo magumu ambayo ameshakutana nayo kwenye maisha yake kwani mwaka 2009 aliwahi kuvamiwa huku akikatwakatwa mapanga na kunyang’anywa hela zaidi ya milioni tisa.
GARI LA POLISI LILILOBEBA WATUHUMIWA LAPATA AJALI GEITA ‘WATU WANNE WAFARIKI DUNIA’