ABDUL JALANA, ni mfano halisi wa kijana anayeithibitishakwa vitendo kanuni ya mafanikio hujengwa kwa jitihada. Kijana huyu aliyezaliwa na kukulia mkoani Mtwara miakathelathini iliyopita, mwenye makazi yake jijini Dar es salaam kwa sasa, amejenga historia inayomgeuza kuwa kioo mbeleya jamii kwa namna anavyojitoa kufuata ndoto zakealizoziamini ni chachu kwa jamii kunufaika nazo.
Kijana huyu amepata elimu katika shule ya msingi nasekondari King David mjini Mtwara. Alipohitimu alifanikiwakujiunga na chuo cha TPA hapohapo Mtwara kinachotoamafunzo mbalimbali yanayohusu shughuli za bandari.
Jitihada zake zimechagizwa kwa misingi imara waliyonayokatika familia yao inayoongozwa na baba yao mzee Jalana. Hivyo anapita nduguze walimopita, lakini yeye anapita kwakishindo kikubwa. Alama anayoiacha ni alama ya moto ambayo ni ngumu kusahaulika.
Utii wa malezi aliyopatiwa umemjengea imani iliyokomazwana wazazi wake waliokuwa wafanyabiashara wa vituo vyamafuta na nyumba za kulala wageni mkoani Mtwara. Imani hiyo ndiyo iliyomsukuma wakati wote kuwa hamnakinachoshindikana hapa duniani zaidi ya kurudisha uhai wamtu aliyefariki.
Imani imemsukuma kutekeleza kila leo, ijapokuwachangamoto za hapa na pale hazikuisha kumwandama. Ameshapitia hatua nyingi ambazo hazikumpa matokeotarajiwa, moja wapo ni ya uimbaji. Alishaimba, na ana nyimbo kadhaa, lakini alichokipata hakikutimizaanachokihitaji hivyo alisitisha kufanya shughuli hiyo.
Huyu ni mtaaluma wa uendeshaji wa mitambo ya upakuajimizigo bandarini, lakini hitaji la moyo limepelekea kuiwekapembeni taaluma hii na kuiinua ile iliyomfanya kuwa namazingatio muda wote. Nayo ni huduma ya ushauri nauendeshaji wa programu za kidijitali.
Bidii aliyonayo imemfanya leo hii kumiliki kampuni mbilizenye mwenendo mzuri sokoni ukizingatia na maono yakampuni husika. Nazo ni; Software Hub na AJ CAR HIRE.
SOFTWARE HUB (@swhagency) | Instagram
Akiwa kama Mkurugenzi, chini ya kampuni hizi; Software Hub, inayojihusisha kutoa huduma ya utengenezaji nauboreshaji wa programu mbalimbali za kidijitali, na AJ CAR HIRE, inayotoa huduma ya ukodishaji wa magari kwamatukio mbalimbali nchini, amedhihirisha mfanowe. Kwamba kukata tamaa ni mwiko.
Hatua kadhaa za hapo nyuma, zinamwingiza kundinilinaloongozwa na Rais wa Jamhuri ya Kenya, William Ruto, kundi la ma-hustler wasiyoyumbishwa na mitazamo hasikutoka nje ya maono yao.
Huduma bora anayoitoa katika kampuni yake ya Software Hub, imemwezesha kuaminiwa na kupewa majukumu yakuongoza na kuwasimamia baadhi ya wasanii wa muziki nafilamu nchini kama Meneja. Wasanii hao ni Baraka Da Prince, Nuh Mziwanda, Kajala Masanja, Petman, Jacqueline Wolperna Harmonize.
Mbali na hawa, amefanya kazi na wasanii wengine, watumashuhuri, taasisi mbalimbali; za umma na binafsi. Kama vile, Malkia Karen, S 2kizzy na ITV. Vilevile amesimamia nakuongoza shughuli za uboreshaji wa kidijitali kwa wadauwengine wa kisiasa, akiwemo Yerico Nyerere-ambaye nimwandishi wa vitabu pia.
Chini ya Software Hub amefanya kazi pia na kampuni yaState Aviation inayojihusisha na shughuli za usafiri wa angakwa kutumia helikopta akiwa mtu wa matangazo. Shughulizote zinazohusu kuitangaza kampuni hiyo kidijitali namabango ipo chini yake.
Amefanya kazi pia na Salim Aziz Salim, ambaye ni Afisamtendaji mkuu wa Bakhresa Food Products Limited na Hotel Verde kupitia huduma ya uwezeshaji wa Azam Pesa hadikufikia ilivyosimama leo hii. Kuziboresha akaunti zao binafsibaadhi ya watendaji wa Azam nayo ni kazi iliyopita chiniyake. Huku akishirikiana kwa ukaribu na Abuu Branding, mtuwa matangazo Azam nzima.
Kufanya vizuri kwa akaunti mbalimbali za mitandao yakijamii ya watu hao ni juhudi za uwekezaji wa akili namaarifa unaofanywa na kijana huyu. Amejitoa kuhakikishajamii inanufaika vyema na kile alichojaliwa.
Wakati akifanya vizuri katika uwanda wa teknolojia na sanaa, imekuwa vivyo hivyo katika usafirishaji. Kwa muda mfupi wahuduma alioutoa kupitia AJ CAR HIRE, yenye ofisi maeneoya Mlimani City jijini Dar es salaam, amefanya kazi namashirika mbalimbali kiasi cha kuwa na mvuto kwa watukadhaa mashuhuri kutoka serikalini na sekta binafsi nchini.
AJ CAR HIRE (@ajcarhire) | Instagram
Kampuni hiyo imetoa huduma bora kiasi cha kushawishiwateja wa nje ya nchi, hasa watalii. Kampuni hii kwa sasaimeweza kuajiri zaidi ya watu kumi; ambao ni madereva nawatu wengine wa ofisini. Huku wateja wake wengi wakiwawatu mashuhuri wanaoondoka na kurudi nchini kwa safari za kwenda uwanja wa ndege.
Kitovu cha kampuni hii kipo Zanzibar.
Matokeo yanayopatikana kwenye kazi zake ndiyoyaliyowahimiza viongozi hawa wampatie heshima ya kipekeena nafasi katika muda wao wa kumfuatilia na kutumiahuduma yake pia.
Miongoni mwa watu hao ni Jakaya Mrisho Kikwete, RaisMstaafu wa awamu ya nne ya serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Joseph Kusaga, Mkurugenzi wakampuni za CMG (Clouds Media Group) na Angelina Mabula, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi nchini.
Kwa pamoja, hawa wameshawishika na kile kinachofanywana Abdul, kiasi cha kukutana na kijana huyo kwa wakatitofauti kubadilishana naye mawazo na kumpa hamasainayozidi kumwongezea morali ya utendaji kazi wake kilauchao.
Mbali na mvuto huo kwa watu wenye nyadhfa, ametengenezahamasa pia ya kufuatiliwa kwa vijana wengi. Kwani mara kwa mara amekuwa msitari wa mbele kutoa ushauri namafunzo mbalimbali kuhusu usalama wa programu za kidijitali.
Juu ya yeye kuvutia wengi, naye amehamasika na mshirikamwenzie, Morris Mbetsa, kijana mbunifu kutoka nchiniKenya, mtu wa kwanza Afrika kutengeneza drone inayowezakubeba mtu mmoja na kupaa kwa kilomita kadhaa. Huyu nimwanateknolojia aliyewezesha ununuzi wa luku uwe unaingiamoja kwa moja pasipo kuweka kwenye mita. Kwa umoja waowamewezesha mawazo hayo kufanyiwa kazi serikalini baadaya kupenyeza ushawishi kwa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, naye kuwasilisha sehemu hitajika. Na sasa matumizi yamawazo yao yamefanyiwa kazi kwa kuona smart meter sehemu mbalimbali nchini.
Abdul amesimika mlingoti imara unaopeperusha vyemabendera ya jitihada inayomwonesha kila kijana haipaswikukata tamaa pasi kujali hatua unazopitia na matokeo yake. Maisha ya Mtwara hayakumchora katika umbo alilonalo sasa, lakini ameweza kusimama imara muda wote na kuoneshauwezo wake, huku akihaidi kurejea kwenye shughuli za muziki alizokuwa amezisitisha.