Kijana Abubakar Ibrahimu(21) Mkazi wa Katundu ameuawa kwa kuchomwa kisu na Kijana mwenzake eneo la Machinjio Wilaya na Mkoa wa Geita chanzo kikiwa ni deni la Tsh. elfu 5.
RPC wa Geita, Safia Jongo amesema Abubakar alikuwa akidai deni la shilingi 5000 baada ya kazi ya kuchinja na kuchuna mifugo katika machinjio ya Serikali Kata ya Mtakuja.
“Walikuwa wanadaiana deni la shilingi 5000 baada ya kazi ya kuchinja na kuchuna mifugo ambayo ilichinjwa yaani hawa ni Wachunaji wako pale machinjio kama Wachunaji kwahiyo baada ya malipo ndio wakaanza kugombania hiyo 5000”
“Mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi huku upelelezi ukiendelea ambapo kwa taarifa za awali Mtuhumiwa huyo alimchoma Abubakari kifuani mara mbili kwa kutumia kisu ambacho alikuwa akikitumia kufanyia kazi hiyo katika machinjio”