Katika pita pita zangu mtandaoni nimekutana na hii mtu wangu, first eleven ya wachezaji bora wa muda wote katika historia ya soka. Yaani nimekutana na list ya wachezaji 11 ambao wamepata nafasi ya kuunda kikosi bora cha muda wote. Hii ni kwa mujibu wa muandishi wa mtandao wa sokka.com Edward Aiko Bua mtu wangu.
1- Ni golikipa wa zamani wa klabu ya Chelsea ila kwa sasa anachezea klabu ya Arsenal ya Uingereza Peter Cech yeye anatajwa kupewa nafasi hii kwa sababu kadhaa ila moja kati ya hizo ni kutokana na kuweka rekodi ya kuokoa michomo mingi zaidi katika historia ya Ligi Kuu Uingereza.
2- Hector Bellerin ni beki wa kulia wa klabu ya Arsenal sifa yake kubwa iliyomfanya awekwe katika list hii, anatajwa kuwa na kasi na uwezo wa kucontrol mpira. Hector anatajwa kuwa na kasi zaidi ya mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt.
3- Beki wa kati nafasi hii imekwenda kwa Franz Beckenbauer, huyu ni mkongwe ambaye alianzia soka lake katika klabu ya FC Bayern Munich na kuustafia katika klabu ya New York Cosmos. Sababu inayomfanya kupewa hii nafasi ana uwezo na mamlaka katika nafasi yake ya beki. Huyu pia ndio jamaa aliyewahi kutwaa Kombe la Dunia kama mchezaji mwaka 1974 na kama kocha mwaka 1990.
4- Sol Campbell anaingia katika list ya wakongwe wa Arsenal waliyowahi kucheza kwa mafanikio klabuni hapo, Campbell ni moja kati ya mabeki wa kati mahiri waliowahi kutokea, hivyo sokka.com wameamua kumjumuisha katika hii list.
5- Roberto Carlos huyu anapewa nafasi ya kucheza beki ya kushoto, uwezo wake na umahiri wake wa kupiga mashutu na faulo kwa mguu wake wa kushoto ndio kuna mfanya apewe hii nafasi. Carlos ni moja kati ya wachezaji wachache wa soka wenye nguvu za miguu.
6- Patrick Vieira huyu sokka.com wanampa nafasi ya kucheza nafasi yake ya kiungo mkabaji kama ambavyo Arsenal walikuwa wanamtumia. Sifa yake kubwa kiungo huyo iliyomfany apewa nafasi hii ni umahiri wake wa kucheza tackling lakini ni mchezaji mwenye faida akiwa na mpira na asipokuwa na mpira.
7- Kiungo mshambuliaji nafasi hii anapewa kiungo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa aliyekuwa anakipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Zinedine Zidane ambaye ni moja kati ya viungo wazuri kutengeneza nafasi za magoli, kama Zadane asingekuwepo nafasi yake angepewa Robert Pires.
8- Mesut Ozil huyu ni kiungo mwingine aliyepewa nafasi ya kuingia katika list hii, Ozil sifa yake kubwa ni master wa kupiga pasi za mwisho(assist) za magoli. Kama Ozil asipokuwepo nafasi yake wangeweza kupewa hawa Baggio, Guardiola, Rivaldo na Figo.
9 – Lionel Messi anapewa nafasi ya ushambuliaji kama ambavyo tumezoea kumuona akiwa katika klabu yake ya FC Barcelona. Uwezo wake na maajabu yake ya kutumia vizuri mguu wake wa kushoto ndio kuna mfanya apewe nafasi hii.
10- Romario huyu ndio mshambuliaji mwingine anayeungana na Lionel Messi kuunda safu ya ushambuliaji ya kikosi hiki. Romario anatajwa kuwa ni miongoni mwa wachezaji hatari ndani ya penati box. Kama Romario akitolewa Raul Gonzalez ndio pekee anapewa nafasi ya kurithi nafasi hiyo.
11- Pele huyu na Maradona ndio wanatajwa kuwa wachezaji bora wa Dunia wa muda wote, licha ya kuwa Maradona hayupo katika hii list ila hawa kwa pamoja wanaingia katika kumbukumbu ya vitabu vya soka vya muda wote. Kikubwa kinachomuweka Pele katika list hii, ndio mchezaji pekee aliyefunga magoli mengi katika maisha yake ya soka sambamba na kutwaa Kombe la Dunia mara tatu.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.