Kikosi cha Msaada wa Haraka cha Sudan (RSF) kimetoa taarifa kikidai kimefanikiwa kushambulia jeshi la Sudan pamoja na washirika wake tarehe 18 katika mji wa Shendi, jimbo la Nile, kaskazini mwa nchi hiyo.
Taarifa imesema katika mashambulizi hayo, kikosi hicho kimewaua askari zaidi ya 300 wa jeshi la Sudan kwa kuwapiga risasi na kukamata askari wengine 25 pamoja na magari zaidi ya 70 ya kivita na silaha nyingi zikiwemo makombora na mizinga. Hadi sasa jeshi la Sudan bado halisema lolote kuhusu taarifa hiyo.