“Mimi mwanasiasa unasema nisome salam fupi, una hatari wewe! ndugu mgombea mie Bagamoyo ni kwetu kwa hiyo niliposikia unakuja kwenye kampeni kwetu na mie ni Mwanabagamoyo kindakindaki kwa kuzaliwa nikaona siwezi kukosa lazima niwepo kuungana na Wanabagamoyo wenzangu, Wanapwani wenzangu kukukaribisha, karibu Pwani, karibu Bagamoyo” Mstaafu Kikwete
“Nakupa pole kwa kazi kubwa unayoifanya ya kampeni, nimeifanya kwa hiyo naijua adha yake, naujua ugumu wake lakini naijua raha yake na raha yake ni hii, unakuwa umechoka sana lakini ukiwakuta watu wamejaa, wana furaha, nyuso zao zina bashasha, roho yako inakuwa baridiii” Mstaafu Kikwete
“Pole, hongera lakini mpaka sasa umefanya kazi nzuri, umeendesha kampeni vizuri na mimi sina wasiwasi utashinda, utasinda sana na chama chetu kitashinda, kitaendelea kuongoza taifa letu, siioni hofu wala sioni sababu ya CCM kushindwa au mgombea wetu wa Urais kushindwa au wagombea wetu wa ubunge wengi kushindwa” Mstaafu Kikwete
“Hilo silioni kwa sababu sioni sababu ya hilo lakini kwanini? Kwa sababu chama chetu chini ya uongozi wako, kimeiongoza vizuri nchi yetu, mambo mengi mazuri yamefanyika na wananchi hilo wanatambua na kwa hilo shukrani yao wataionyesha tarehe 28 kwenye sanduku la kura” Mstaafu Kikwete
“Endelea kupambana lakini endelea ukiamini hakuna litakaloharibika, Tanzania ilivyo leo sivyo ilivyokuwa 2015 wakati nakukabidhi nchi, tumepiga hatua kubwa ya maendeleo, nchi ni tulivu, jamani tunataka nini tena? nani kama CCM, nani kama Magufuli? Asante sanaRais, karibu sana” Mstaafu Kikwete