Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, ameonesha kushangazwa na maamuzi ya Rais Magufuli, baada ya kumfukuza mfanyakazi Msukuma wa Ikulu, ambaye alishindwa kununua incubator ya kutotoa mayai ya Tausi.
Kikwete ameyabainisha hayo leo Dodoma, wakati wa zoezi la kukabidhiwa ndege aina ya Tausi kwa Marais wastaafu pamoja na mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere.
“Mimi ndiyo mdogo nasema kwa niaba ya Wazee hawa, tunatoa shukrani kwa moyo wako wa upendo kwa kutupatia hawa ndege, tulikuwa tunawatamani lakini ukitoka nao, ukafika nao Msoga, watu watasema amepora, pia nakupongeza kwa maamuzi ya incubator lakini yule Msukuma sikukuambia umfukuze, lakini nilieleza tu masikitiko yangu” Dkt. Kikwete
#LIVE: MAGUFULI “KIKWETE ALIMCHONGEA MSUKUMA HAWEZI, NIKAMFUKUZA IKULU”