Unaweza ukafikiri labda dawa ya kuondoa unene ni kufanya mazoezi, kula vyakula vyenye mpangilio pekee, kupunguza uzito na vitu vingine ila la hasha utafiti unaonyesha sio hivyo tu. Hii ni makala maalumu ya ambayo imezungumzia mambo matano ya kushangaza yanayosababisha kuongeza uzito wa mwili.
1. Bakteria ndani ya Utumbo
Unaambiwa achilia ya kuwa na uzito wa namna gani, wanasayansi wanaamini kwamba utofauti wa kilo za watu unatokana na bakteria za mwilini wanaoishi ndani ya utumbo, mfano uchunguzi ulifanywa kwa mapacha wawili kwa zaidi ya miaka 25, ambapo mmojawapo ana kilo 41 zaidi ya mwenzake na matokeo ya utafiti yanaonyesha kwamba utofauti wa vinyesi vyao umeonyesha kwamba pacha aliyemwembamba alikua na bakteria wa aina tofauti huku mwenzie mnene naye alikua na bakteria fulani ndani ya utumbo wake.
”Iwapo wewe ni mnene sana , basi huenda huna aina nyingi za bakteria kama inavyostahili katika utumbo wako’‘ anasema profesa huyo ambaye amegundua mtindo wa aina hiyo katika utafiti wa watu 5000.
2. Vinasaba tunazorithi
Wanasayansi katika chuo kikuu cha Cambridge wanaamini kati ya 40-70% ya athari ya uzito wa miili ya watu unatokanana na utofauti wa vinasaba ndani ya mwili. Hivyo unaweza kuwa unakula lishe bora lakini bado ukawa haupunguzi unene.
3. Muda unaokula chakula
Kuna ukweli katika msemo wa zamani kwamba kula kiamsha kinywa kama mfalme, chakula cha mchana kama Lodi na cha usiku kama masikini, lakini sio kwa sababu unazozifikiria. Watu wengi wamekua wakila bila mpangilio maalumu
Mtaalamu wa kuhusu masuala ya unene wa mwili Dkt James Brown anasema kila tunapokula kwa kuchelewa basi tuna nafasi kubwa ya kuongeza kilo mwilini na sio kwasababu usiku ni muda wa mapumziko na hatuna shughuli nyingi kama inavyoaminika na wengi, lakini ni kwa sababu ya saa zetu za ndani ya miili.
Inapofika usiku miili yetu hupata shida kusaga chakula – mafuta na sukari kwahivyo unapokula chakula chenye mafuta kabla ya saa moja usiku huenda kukakusaidia kupunguza kilo au kukusaidia kukuzuia kuongeza kilo mwilini.
4. Kuudanganya ubongo wako
Kuna namna tofuati za kubadili namna tunavyokula chakula na sio tu kutegemea kuhesabu kiwango cha kalori ndani ya chakula tunachokula, kwa mfano kuondoa vishawishi vya vyakula ni bora zaidi kuliko kutegemea kuacha, Hivyo unashauriwa kutoweka vitu vitamu jikoni kwako vitakavyosabbaishia kupata vishawishi badala yake ni bora uweke matunda.
Ka mfano unaweza ukawa unaangalia TV hapo usikae na pakti nzima ya biskuti huku ukiangalia TV, bali weka kiwango unachotaka kula kwenye sahani na usiongeze zaidi ya hapo.
5. Homoni
Kubadilika kwa hamu ya kula chakula kunadhibitiwa na homoni ndani ya mwili na hivyo imegunduliwa kwamba kuna upasuaji wa kuufunga utumbo – maarufu kama bariatric surgery – kunasaidia kuunda homoni nyingi zinazotufanya kuhisi kushiba kuliko homoni zinazotufanya kuhisi njaa ambazo hupungua.
Lakini ni upasuaji mkubwa unaohusu kupunguza ukubwa wa tumbo kwa hadi 90% na hufanyiwa watu wenye BMI ya 35 au zaidi pekee na mgonjwa hudungwa mchanganyiko wa homoni 3 katika sindano kila siku kwa wiki nne.
“Mtu haisi njaa sana, wanakula chakula kidogo na wanpunguza kilo kati ya 2-8kg katika muda wa siku 28 ,” anasema mtaalamu Dkt Tricia Tan.
Jinsi binti alivyotumia YouTube kujizalisha mwenyewe