Kuanzia mwaka huu, kila mtoto anayezaliwa huko Illinois nchini Marekani atakuwa na dola 50 zaidi ya Sh. 117,000 iliyowekwa kwenye akaunti ya akiba ya Chuo Kikuu.
Uwekezaji huo mdogo ni sehemu ya sheria mpya ambayo inaanzisha Mpango wa Akiba ya Elimu ya Juu ya Illinois, ambapo wabunge wana matumaini kuwa itahimiza familia kuanza kuweka akiba kwa ajili ya elimu ya mtoto wao mapema na kuruhusu pesa hizo zikue.
Pesa hizo zinaweza kutumika katika vyuo vya jadi vya miaka minne, shule za ufundi, vyuo vya miaka miwili na taasisi zingine.