Kila mwaka, watanzania na Raia kutoka pembe zote za dunia hukutana Moshi kule Kilimanjaro kushiriki mashindano ya mbio maarufu “Kili Marathon” ambayo yanathaminiwa na Tanzania Breweries Limited (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager. Kilimanjaro Lager imekuwa ikidhamini hafla hiyo na kuleta kiburudisho kwa watanzania huko Moshi kwa miaka 18 sasa.
Mnamo Machi mwaka huu, Kilimanjaro Premium Lager iliamua kufanya vitu tofauti na ikaanzisha kwa mara ya kwanza, teknolojia ya upigaji picha ya hali ya juu wakati wa mbio hizo. Teknolojia hii iliyoandaliwa na Kampuni ya AIMGroup Tanzania, inajulikana kama Kili Photo Canvas na ni mfumo wa kipekee ambao ulipiga picha za waimbiaji wakati walikuwa wanakimbia mbio za Kili marathon na kuwatumia moja kwa moja kwenye simu yao kupitia WhatsApp. Hii imeiweka bia hiyo kama kiongozi wa uvumbuzi ulimwenguni.
Teknolojia hii iliwezesha mkimbiaji kufurahia mbio hizo na iliwapa kumbukumbu na urahisi kwa kushare kumbukumbu hizo na marafiki na familia kupitia mitandao ya kijamii. Wale ambao walishiriki katika mbio za mwaka huu za Kili, wanaweza kutazama picha zao na kupakua picha zao http://kililager.com Kwa kuingiza nambari yako ya simu utaweza kuona picha zako na unaweza kupakua mzigo wote. Unaweza kushare familia yako na marafiki kwa kutumia #JiachieNaKiliMarathon kwenye mitandao ya kijamii. Usisahau kuweka tag @kili_lager.
Ili kuwezesha zoezi hili, Bia ya Kilimanjaro Premium lager iliandaa mashindano ya uchoraji ambapo wasanii 35 kutoka Tanzania nzima, walitengeneza michoro kwa kutumia baadhi ya vitu vilivyo kwenye chupa ya Kilimanjaro Premium Lager na mlima wa Kilimanjaro. Washindi walipewa TZS. 2,000,000 kama zawadi na michoro yao ilitumika kama wallpaper kwenye Kili Photo Canvas. Ili kufikia watu wengi zaidi, michoro iliwekwa katika maeneo mbali mbali jijini Dar es salaam na Moshi na kila wakati wakimbiaji walipopita mbele ya michoro hiyo, walipata kupigwa picha na wakaipata picha yao moja
Kulikuwa na amsha kubwa wa umma na watu 2,144 waliojiandikisha kushiriki na picha 2700 zilizopigwa na kushirikishwa katika kumbukumbu za kilimarathon 2020
Angalia video ya Kili Photo Canvas hapa chini