Hatimaye hatua ya 8 bora ya michuano ya kombe la dunia imeanza leo kwa michezo miwili kati ya Brazil dhidi ya Colombia na ufaransa dhidi ya Ujerumani.
Kwenye mchezo wa kwanza Ujerumani ilifanikiwa kuifunga Ufaransa 1-0 kwenye mchezo mkali uliozikutanisha timu hizo, goli la beki wa Borrusia Dortmund Matt Hummels alilofunga kwa kichwa katika kipindi cha kwanza likaipeleka Ujerumani nusu fainali ya tatu mfululizo tangu mwaka 2006.
Mchezo wa pili ulizikutanisha Brazil ambao ni wenyeji dhidi ya majirani zao Colombia.
Magoli ya mabeki Thiago Silva na Rafiki yake wa tangu utotoni David Luiz yakaipeleka Brazil kwenye nusu fainali dhidi ya Ujerumani.
Colombia walipata goli lao la kufutia machozi kupitia mkwaju wa penati wa mshambuliaji James Rodriguez, moaka refa anamaliza mpira Brazil 2-1 Colombia.
Mechi za kesho ni Belgium
Vs Argentina saa 1 usiku na Costa Rica vs Holland hii itakuwa saa 5 usiku.