Wakazi wa Arusha, wanaozunguka eneo lilotengwa kwa ajili ya ujenzi wa stendi mpya ya Bondeni City, wamemwomba Rais Samia kuingilia kati mgogoro wa sehemu pakujengwa stendi hiyo, unaoongozwa na baadhi ya wanasiasa wa Mkoa huo.
Wakizungumza na waandishi wa habari wakiwa katika eneo la ujenzi wa stedi hiyo, kwa niaba ya wananchi wa eneo hilo,Hawa Ramadhani na Masai Ngetua, walisema wanataka stendi hiyo kujengwa eneo la Bondeni City.
“Kumekuwapo na taarifa kwamba ujenzi wa stendi unataka kuhamishiwa huko Olasiti kwa kweli hatutafurahishwa na kitendo hicho, kwa kuwa sisi tunataka stendi ijengwe hapa Bondeni City.
“Tunamwomba Rais Samia kuingilia kati mgogoro huu kwa kuwa wako baadhi ya wanasiasa wanataka stendi kuhamishwe kwenda kujengwa Olasiti kwa kuwa wana maslai yao binafsi iliha kuna eneo la bondeni city ambalo linafaa kwa ujenzi.alisema Ngetua.