Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama imekamata Kilogramu 4.623 za aina mpya ya dawa ya kulevya inayoitwa methylene dioxy pyrovalerone (MDPV) iliyokamatwa jijini Dar es Salaam ikisafirishwa na raia wa Comoro anayeitwa Ahmed Bakar Abdou (32).
Methylene dioxy pyrovalerone (MDPV) ni dawa mpya ya kulevya iliyo katika kundi la vichangamshi inayotengenezwa kwa kutumia kemikali bashirifu.
Dawa hii ina kemikali inayoweza kuleta madhara ya haraka kwa mtumiaji ikilinganishwa na dawa nyingine za kulevya. Pia, imeongezwa nguvu ya kilevi inayozidi cocaine, methamphetamine na heroin .
Aidha, dawa hii ya kulevya huuzwa kwa njia ya mtandao (internet) na husafirishw kupitia kampuni za usafirishaji vifurushi na hufichwa kwa kuwekwa chapa za majir bandia kama vile bath salts, Ivory Wave, plant fertilizer, Vanilla Sky, na Energy