Kim Jong-un ameendelea kumweka bintiye kwenye uangalizi baada ya kwenda naye kwenye ziara ya kituo cha anga za juu cha Korea Kaskazini.
Mtoto wa dikteta huyo, Kim Ju-ae, alikuwa pembeni yake huku pichani wakionyeshwa maeneo tofauti ya makao makuu ya anga ya nchi.
Si mara ya kwanza kwa binti huyo mwenye umri wa miaka 11 kuwa na kiongozi huyo katika miezi ya hivi karibuni, huku wawili hao wakijitokeza pamoja mara kwa mara kwa matukio na majukumu na umekuwa muonekano wa kawaida kwani wote walionekana wakitazama mechi maalum ya kumbukumbu ya miaka kwenye picha zilizotolewa jana.
Wiki iliyopita tu, familia nzima ya Kim ilikusanyika kutazama jaribio la kombora lenye nguvu zaidi la Korea Kaskazini wakati huo huo, Kim Ju-ae alipigwa picha akiwa ameketi kando ya baba yake kutazama jeshi likiiga shambulio kwenye uwanja wa ndege wa Korea Kusini.
Uvumi umeendelea kuhusu iwapo anaandaliwa kumrithi babake kama dikteta ajae wa nchi hiyo katika siku zijazo.
Katika ziara hiyo, Kim Jong-un alisema Korea Kaskazini imekamilisha utengenezaji wa satelaiti yake ya kwanza ya kijasusi wa kijeshi, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya serikali leo.
Maafisa wameagizwa kuendelea na uzinduzi kama ilivyopangwa na Kim Jong-un, ambaye alisema kuendeleza upelelezi ni sehemu ya juhudi za taifa hilo kukabiliana na ‘matishio makubwa ya kiusalama’ kutoka Marekani na Korea Kusini.