Huenda hofu ya kuambukizwa virusi vya Corona ndio imesababisha kutoonekana hadharani kwa Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, kauli hii imetolewa na Waziri wa Muungano wa Korea ya Kusini baada ya uvumi kuhusu afya ya kiongozi huyo.
Kwa upande wake Rais Trump amesisitiza tena kwamba Kim ni mzima na hakuna tatizo lolote linalomsumbua na kwamba muda si mrefu atajitokeza hadharani.
“Kuhusu Kim Jong Ung, siwezi kuwaambia kwa undani, lakini nafahamu kinachoendelea kumuhusu ila siwaambii chochote kwa sasa, namtakia tu kila la kheri huko aliko, nina mahusiano mazuri sana na Kim, kama nisingekuwa Rais wa Marekani, USA ingekuwa kwenye vita kubwa na Korea Kaskazini, Kim ni mzima na siku sio nyingi mtasikikia taarifa zake”– TRUMP
BREAKING: VIFO VYA CORONA TANZANIA VYAFIKIA 16, JUMLA YA MAAMBUKIZI 480, WALIOPONA 167