Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kimbunga Ialy kinachoendelea kuvuma kaskazini mwa Madagascar, ambacho awali kilitabiriwa kuwa kingeishia baharini, kinaendelea kupata nguvu na kinatarajiwa kusababisha mvua kubwa na upepo mkali nchini Tanzania siku ya Jumanne Mei 21,2024.
Taarifa iliyotolewa imesema kimbunga hicho kilichopo umbali wa kilomita 680 kutoka pwani ya Tanzania, kitasababisha mvua kubwa na upepo mkali unaozidi kasi ya kilomita 40 kwa saa na mawimbi yanayozidi mita 2 , huku mvua kubwa ikitabiriwa kunyesha katika maeneo ya pwani hadi jumatano ya Mei 22.