Katika kuhakikisha Watanzania wanakumbushwa kuchukua tahadhari dhidi ya utabiri wa uwepo wa kimbunga Jobo, Mamlaka ya hali ya hewa ilisema jana kuwa kimbunga hicho leo Jumamosi mchana April 24 kilitarajiwa kuwa umbali wa kilometa 125 Mashariki mwa Mafia.
Taarifa hiyo ilisema pia usiku wa leo ambao ni wa kuamkia Aprili 25, kinatarajiwa kuendelea kupungua nguvu kikiwa katika mwambao wa Pwani ya Tanzania.
Vipindi vya upepo mkali unaofikia kilometa 50 hadi 60 kwa saa, mawimbi makubwa baharini pamoja na ongezeko la mvua kwa maeneo ya ukanda wa Pwani vinatarajiwa kujitokeza.
Maeneo yanayotarajiwa kupata athari za moja kwa moja kutokana na kimbunga Jobo ni Kisiwa cha Mafia, Lindi, Dar es Salaam, Unguja, Mtwara, Tanga na Pemba.
UJENZI DARAJA LA JPM KUKAMILIKA KABLA YA WAKATI, WEZESHI LAKAMILIKA 100%
https://youtu.be/5vNscwNMzYE