Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei ambaye sasa ni mteule wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Ubunge wa Jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro amesindikizwa na umati kurudisha fomu katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Mjini Moshi.
Akizungumza baada ya kukabidhi fomu kwa Tume ya Uchaguzi mjini Moshi, Dr. Kimei ambaye ni mchumi mbobevu, amesema kuwa imani kubwa iliyopo kwa Rais Magufuli pamoja na yeye kama mgombea vimewapa matumaini mapya wana vunjo.
“Nakishukuru sana Chama changu cha Mapinduzi CCM, chini ya Mwenyekiti Dr. John Pombe Magufuli, kwa kuniamini na kunipa nafasi ya kugombea kuwawakilisha wana Vunjo” Kimei
“Hii ni heshima kubwa sana kwang nawasihi wana Vunjo wote tuungane kwa maslahi mapana ya jimbo letu la Vunjo ili tulete maendeleo kwa kizazi kilichopo na kijacho, napenda kuanza na shukrani kwa kila mtu aliyewezesha kuanza safari hii” Kimei
“Siku chache zijazo nitaeleza kwa undani mpango mkakati wangu, ambao naamini kwa kushirikiana na kila mwenye kuitakia mema Vunjo, tutafanikiwa, pamoja tunaweza ” Kimei
MBWEMBWE ZA KIMEI ALIVYOFIKA OFISI ZA MKURUGENZI KUREJESHA FOMU VUNJO