Katika mataifa ambayo hayako kwenye uhusiano mzuri duniani ni Marekani na Korea Kaskazini, Kim Jong-Un ambaye ni Rais wa Korea Kaskazini amekuwa akitajwa kama mmoja ya viongozi ambao hawatabiriki kwenye suala la maamuzi, anaamua chochote atakachojisikia kwa wakati wowote.
Siku ya March 8 dunia nzima ilisherehekea siku ya wanawake Duniani, watu wakapeleka zawadi kwa dada zao, ndugu zao wa kike, lakini mlengwa mkubwa alikuwa mama.
Rais wa Korea nae alikuwa na zawadi kwa wanajeshi wake wanawake ambao wako kwenye Kambi ya siri ya Jeshi la nchi hiyo, katika ziara yake hiyo amegawa vitu kadhaa kwa wanajeshi hao ikiwemo vipodozi vya wanawake kama vile poda na vingine.
Japo Kim hakukutana na wanajeshi hao mmoja mmoja lakini mzigo wa zawadi hizo ulifikishwa kwa Mkuu wa Kambi hiyo na kuagizwa kwamba ni zawadi ambazo zinatakiwa kumfikia kila mwanamke ambaye yuko kwenye kambi hiyo.
Wewe ulimpa zawadi gani mama yako? Unaweza kuniandikia yako hapa mtu wangu lakini Rais Kim yeye katoa zake vipodozi yani.