Kachumbari ni hatari….imeelezwa kwamba Ulaji wa kachumbari katika kuongeza ladha ya chakula ni jambo hatari iwapo nyanya na mazao mengine ya kutengeneza kiungo hicho maarufu yatakuwa na viambata vya sumu vinavyotokana na viatilifu vinavyotumiwa na mkulika shambani.
Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na mtafiti kutoka mamlaka ya ya afya ya mimea na viatilifu (TPRI) Bwana Ramadhani Kilewa wakatika akitoa mafunzo ya siku tatu kwa maafisa ugani wa wa Bens Agrostar company Ltd,waliotoka mikoa mbalimbali nchi.
Kwa mujibu wa mtafiti huyo ameeleza kwamba kwa kawaida nyanya na mazao mengine yana takiwa kukaa shambani kwa siku hadi 21 baada ya kunyunyiziwa viatilifu vya kuua wadudu na visumbufu vya mimea kwa ujumla ilikupisha viatilifu hivyo kufanya kazi yake sawasawa kabla yakuwa tayari kwa malaji.Kinyume na hapo kwa kukosa Elimu na maadili mazuri mazao hayo yakivunwa kabla ya wakati sumu ya kuua wadudu mojakwamoja humdhuru mtumiaji na matokea yake kusababisha mrundikano wa magonjwa ndani ya mwili wa mtumiaji kama vile saratani na mengineyo.Aidha utupwaji holela wa viwekeo vya viatilifu hivo huwa na madhara kwa mazingira kwakuwa zipo sumu zilizondani ya viatiliafu hivyo kuweza kukaa kwa muda murefu katika mazingira na vingine vinauwezo kupenya hadi kwenye vyanzo vya maji na hivyo kisababisha athari kwa mazingira na afya kwa ujumla. Hivyo kwa kutambua umuhimu wa afya ya mlaji na usalama wa mazingira Bwana Ramadhan Kilewa ameseme serikali imeweka sheria inayo elekeza mafunzo kufanyika kwa wadau wote wa kilimo hususani katika matumizi sahihi ya viatilifu.Pia emeipongeza Bens Agrostar company ltd kwa kutoa mfano mzuri wa kuendesha mafunzo hayo hayo kwa maafisa ugani wake watakao kwenda katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ili kuwasaidia wananchi kwa ujumla hadi vijijini juu yamatumizi sahihi ya sumu za kuua visumbufu vya mimea (viatilifu) ili kilinda Afya ya mlaji kulinda mazingira na kuongeza tija katika kilimo kwa ujumla.
Bwana Patric Mwalunenge ambaye ni mkurugenzi wa biashara wa masoko BENS AGROSTAR CO LDT amesema kuwa semina hii imekuwa ni ya lazima na ni mihimu kwaajili ya kutatua kero za wakulima hasa malalamiko ya wakulima kukutana na viatilifu feki jambo ambalo halina ukweli bali ni kukosa elimu sahihi ya matumizi hayo ya viatilifu.
Kwa upande mwingine meneja wa kampuni hiyo Neema Macha ameeleza kwa kutambua umuhim mafunzo hayo wanategemea kufanya tena kwa aawamu nyingine angalau baada ya miezi sita ili kuwapa uwelewa zaidi wafanayakazi wao hatimaye kumsaidia mwananchi namna nzuri ya kushughulika na viatilifu.
Naye Godliver Rwegoshola ambaye ni asafisa ugani aliyehudhuria mafunzo hayo amepongeza uwepo wa mfaunzo hayo kwakuwa yamewajengea uwezo zaidi na kuishauri serikali kupitia Raisi Samia Suluhu Hassan kuendelea kujenga mazingira wezeshi ya elimu na vitendea kazi ikiwemo upatikanaji wa viatilifu kwa bei nafuu zaidi kwa wakulima vijijini ambapo wamo wakina mama ambao mara nyingi ni nguzo za familia zao huku kilimo ikiwa ndio njia yao ya kujipatia kipato.