Meneja wa zamani wa Manchester United na Uholanzi Louis van Gaal amesema amestaafu kazi ya ukufunzi baada ya miaka 26 katika taaluma yake. Van Gaal, 65, hajafanya kazi uwanjani tangu alipopigwa kalamu na United saa chache baada ya kushinda kombe la FA mwezi Mei 2016.
Akiongea na jarida la Telegraaf la nchini Uholanzi Van Gaal amesema ”Mambo mengi yametokea kwa familia yangu, unakuwa binadamu kwa mara nyingine kwa kukiri ukweli, kwa fikra zangu nilidhani nitastaafu, nikafikiria pia itakuwa ni mapumziko ya muda, lakini kwa hivi sasa sidhani kama nitarudi kwenye kazi ya ukocha,” Van Gaal
Van alitangaza uamuzi wake siku ya Jumatatu baada ya kupata tuzo ku katika taaluma yake kutoka kwa serikali ya Uholanzi kwa mchango wake katika soka. Alisema shida za kifamilia ndizo zilichangia uamuzi wake huo, huku gazeti la De Telegraaf likisema uamuzi wake ulichangiwa na kifo cha mkwe wake mwezi Disemba.
Van Gaal pia alikuwa kocha wa klabu ya Ajax, Barcelona, Bayern Munich, AZ na Manchester United ambayo ilikuwa club yake ya mwisho kuifundisha msimu uliopita. Mbali na kuwa kocha, Van Gaal pia amewahi kuzichezea club za Ajax, Royal Antwep, Telstar, Sparta Rotterdam na AZ.
Raia huyo muholanzi ameweka wazi kuwa alikataa nafasi nzuri za kuendeleza taaluma yake kwa kukataa kazi mataifa ya Mashariki ya Mbali.