Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam imewasihi Wanawake waliokopesha na manispaa hiyo kurejesha mikopo ili wengine wawezw kukopesheka.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Stella Msofe ambaye ni Katibu Tawala wa Manispaa hiyo pia amewasihi wanawake kujikita kuongeza maarifa na ujuzi wa vitu mbalimbali.
“Wanawake wenzangu ipo kauli mbiu inayotuongoza inayosema Wekeza kwa Wanawake kuharakisha Maendeleo ya Taifa kwa Ustawi wa Jamii, kauli mbiu hii imebeba ujumbe wa kutosha sana kwamba endapo mtu yoyote ataamua kuwekeza kwa mwanamke atalete ustawi kwa jamii na tunapoizungumzia jamii ni kila kitu kilichopo,
“Kwahiyo niwapongeze sana nyinyi kuwa wanawake lakini kubwa zaidi kuhudhuria siku hii, tumepita katika mabanda na kuona namna gani Halmashauri ya Kinondoni ilivyowekeza kwa wanawake hawa, kubwa zaidi nimpongeze Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha kwamba wanawake wanaendelea kutengeezewa mazingira wezeshi juu ya kuweza kujikwamua kiuchumi kwani anapambana usiku na mchana na hawezi kulala kwani yeye ni Mama wa Taifa hili,”
“Kingine niwasihi sana wale wanaokaa na fedha zetu huko za Manispaa wazirejeshe ili wengine nao waweze kukopesheka,”