Mbabane Swallows licha ya kocha wao Kinnah Phiri siku moja kabla ya mchezo wao wa CAF Champions Leagu dhidi ya Simba SC, kukiri kuwa wamepokea vizuri na Simba SC lakini ukarimu wa Simba SC uliishia nje ya uwanja na ndani ya uwanja waliaadhibu kwa magoli 4-1, kitu ambacho Phiri hakuamini kama kikosi chake cha Mabingwa wa Swaziland kitafungwa hivyo.
Baada ya mchezo Kinnah Phiri aliongea na waandishi wa habari na kueleza kuwa Simba SC, hawakustahili kushinda magoli yote ni vile Mbabane Swallows wamepata bahati mbaya tu katika mchezo huo, Kinnah ameeleza kuwa bado wanayo nafasi ya kusonga mbele licha ya kipigo hicho kwani wana dakika zaidi ya 90 za mchezo wa maruadiano.
“Ninachoweza kusema kuhusu mchezo ni kuwa ilikuwa bahati mbaya kwetu, kwa sababu magoli waliyofunga hawakustahili kufunga lakini katika mpira unafanya makosa mengi na unaadhibiwa sana wameshinda manne na tumeshinda moja ugenini na tuna tofauti ya magoli matatu na wanakuja kwetu, magoli matatu sio mengi sana tunaenda kupambana tena tumejua madhaifu yetu”>>>Kinnah Phiri
EXCLUSIVE: Kauli ya Singida United kushindwa kulipa wachezaji, mbona wanasajili?