Ikiwa zimepita siku kadhaa tangu kutokea kwa kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi, Ayo TV na millardayo.com imefanya exclusive interview na Mbunge wa Muleba kusini na Waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Prof. Anna Tibaijuka ambaye ni miongoni mwa watu waliowahi kufanya kazi za kushirikiana na Marehemu Dr. Mengi.
Prof. Anna Tibaijuka akimzungumzia Marehemu Dr. Reginald Mengi “Mengi alikuwa na elimu bora kabisa na alisomea Ulaya, watu wote sisi tuliosoma Ulaya ni kizazi ambacho tumeshaosha vyombo, tumesafisha barabara lakini vijana wa siku hizi wanachagua kazi”
Prof. Tibaijuka alivyoulizwa kuhusu yanayoendelea mitandaoni kwamba kuna utata wa kifo cha Marehemu Mengi “Vija wautumie muda wao vizuri lakini sasa wapo kwenye maneno ya ajabu sana marehemu Mengi bado hajapata nafasi ya kupumzika katika nyumba yake ya kudumu lakini watu wapo kwenye maneno ya ajabu na huu ninaita ujinga…! ”